Kaa Kimya, Sio Kila Mtu Yuko Timu Yako
Kuna nguvu kubwa katika kunyamaza wakati kila mtu anataka kujua unafanya nini. Watu wengi hupoteza mipango yao kwa sababu wanaitangaza kabla ya kuitekeleza. Wanasema, wanaeleza, wanajivunia kabla hata ya kuanza. Kisha wanashangaa kwa nini baraka zao zinachelewa au kwa nini watu wanaanza kuwazuia bila hata kujua sababu.
Sio kila mtu anayekupigia makofi anataka uendelee. Kuna wale wanaokushangilia kwa nje lakini ndani wanahesabu muda utakapoanguka. Hawa sio maadui wa wazi, ni watu wa karibu, ndugu, marafiki, hata wafanyakazi wenzako. Wanakuwa karibu nawe kwa faida ya kujua unapofikia wapi, sio kwa sababu wanataka ufike mbali.
Kunyamaza sio udhaifu. Ni ulinzi. Mtu anayenyamaza anajilinda mwenyewe kutokana na macho ya wivu na masikio ya uongo. Mipango mizuri hukua gizani kabla ya kuonekana mwangazani. Mbegu haioteshwi juu ya udongo, huzikwa kwanza chini ambako hakuna anayeiona.