Kila Mtu Anataka Uhuru, Ni Wachache Wanaotaka Nidhamu Inayoujenga
Kila Mtu Anataka Uhuru, Ni Wachache Wanaotaka Nidhamu Inayoujenga
Karibu kila mtu anaota maisha ya uhuru: kuwa na muda wako mwenyewe, kuchagua unachotaka kufanya, kutokuwa na mtu wa kukuamuru, na kuishi maisha unayoyataka bila vikwazo. Lakini ukweli mchungu ni huu, watu wengi wanataka matunda ya uhuru, lakini ni wachache sana wako tayari kulipa bei ya nidhamu inayohitajika ili kuufikia. Hii ndiyo biashara nzima ya maisha, unabadilishana nidhamu ya leo na uhuru wa kesho.
Uhuru unavutia kwa sababu ya picha inayotokea akilini: kuamka bila saa ya kengele, kufanya kazi unayopenda, kuwa na uwezo wa kifedha wa kuchagua badala ya kulazimika, na kutokuwa na deni wala mzigo wa lazima. Kila mtu anajua namna uhuru unavyosikika vizuri, hivyo si ajabu kuwa ndilo lengo la wengi.