Tai Haangalii Kipepeo
Watu wengi wanataka mafanikio makubwa, lakini masaa yao yanatumika kufuatilia vitu vidogo visivyo na maana.
Tai haangalii kipepeo. Analenga mawindo makubwa, anaruka juu zaidi ya wale wanaovutiwa na kila kitu kinachopita mbele yake. Ndiyo maana anafika mahali ambapo ndege wengine hawafiki.
Kila siku, kuna vitu vidogo vinavyovutia macho yetu, ujumbe usio na maana, mazungumzo yasiyokuwa na thamani, watu wanaotafuta muda wako bila kuwa na mchango wowote katika maisha yako. Vitu hivi ni kama vipepeo, vinang'aa, vinavutia, lakini havikupi chakula cha kudumu.