Bei ya Kufikiri Tofauti na wajinga

Ukifikiria tofauti na umati, ukikataa kufuata mkumbo, au ukisimama kwa msimamo unaogusa mantiki, kuna uwezekano mkubwa utachukiwa na baadhi ya watu. Sio kwa sababu umekosea, bali kwa sababu wewe si kama wao.

Watu wasiofikiri kwa kina hawapendi kuona mtu anayefikiri kwa kina. Kuwepo kwako pekee kunawakumbusha kile ambacho wao hawajawahi kufanya, kuuliza maswali, kuchambua mambo, kutokubali kila kitu kinachowasilishwa bila kuhoji. Badala ya kujifunza kutoka kwako, wanachagua kukuchukia, kwa sababu ni rahisi zaidi kukulaumu kuliko kubadilika wao wenyewe.

Kila mtu mwenye msimamo wa maana amewahi kukutana na chuki isiyo na sababu ya wazi. Watu wanaokukosoa bila hoja, wanaokuita majina bila ushahidi, wanaokataa kukusikiliza kabla hata hujamaliza kuzungumza. Chuki hii mara nyingi si kuhusu wewe, ni kuhusu wao wenyewe na hisia zao za kutokutosheleza.

Read this on Guava