Mahali Panapotisha Zaidi ni kubaki pale Pale Ulipokuwa Mwaka Jana

Watu wengi wanaogopa mambo makubwa, kuanguka, kudharauliwa, kupoteza pesa, kuanza upya. Lakini kuna hatari kubwa zaidi ambayo watu wachache wanaiona, ni kubaki mahali pale pale kwa muda mrefu bila mabadiliko yoyote.

Fikiria mwaka uliopita. Ulikuwa na ndoto gani? Ulipanga kufanya nini tofauti? Sasa jiulize, mwaka huu, umefika wapi ukilinganisha na mahali ulipokuwa?

Kama jibu ni mahali pale pale, hilo linapaswa kukutisha zaidi kuliko hofu yoyote nyingine. Kwa sababu maisha hayasimami. Muda unaendelea kwenda, watu wengine wanasonga mbele, fursa zinabadilika, lakini wewe unabaki umesimama mahali ulipokuwa.

Read this on Guava