Kwa Nini Kuelewa Watu Ni Bora Kuliko Kuwahukumu
Umewahi kushangazwa na tabia ya mtu, ukajiuliza "kwa nini amefanya hivyo?" Robert Greene, kwenye kitabu chake The Laws of Human Nature, anajaribu kukusaidia kuelewa mizizi ya tabia za binadamu, badala ya kuhukumu tu unachokiona juu juu.
Greene anasema watu wengi tunakosea kwa kuhukumu vitendo vya wengine bila kuelewa nini kinaendelea ndani yao. Kwa mfano, mfanyakazi mwenzako anayeonekana mwenye wivu kila mafanikio yako yanapoongezeka, huenda si mtu mbaya, bali anaendeshwa na hofu ya kutostahili au kuhisi hayupo salama kazini. Ukielewa hilo, unaweza kushughulikia hali kwa hekima badala ya hasira.
Kitabu kinaeleza kuhusu tabia ya "narcissism," yaani kujipenda mno. Greene anasema kila mtu ana kiasi fulani cha kujipenda, lakini wengine wanaipitiliza hadi kushindwa kuona hisia za wengine. Kutambua dalili hizi mapema kunakusaidia kujilinda kabla ya kuumizwa katika mahusiano au kazi.