VIPIMO VYA KUPIMA IQ, VINA HISTORIA NZITO.
SIRI NZITO ILIYOJIFICHA NYUMA YA VIPIMO VYA AKILI (IQ).
Mara nyingi tumekuwa tukiona vipimo vya akili vikitumika kupima ni kiasi gani mtu
ana uwezo wa kufikiri. watu wenye IQ kati ya 100 and 129 wanakadiriwa kuwa watu wakawaida (Jamii kubwa ya watu ipo hapa), watu wenye IQ kati ya 130 na 159 huwekwa kwenye kundi la watu wenye akili kubwa, na watu wenye IQ kuanzia 160 na kuendelea, hutambulika kama watu wenye akili ya juu zaidi, ambapo unakuja kuwapata watu maarufu kama Albert Einstein, Nicola Tesla, Isack Newton, Galileo Galilei n.k watu hawa ndio tunawaita geniuses. na wale wenye IQ chini ya 100 ndio wanatambulika kama vilaza (Hawa nao pia ni wachache).