Ukweli Kuhusu Jinamizi: Kwa Nini Mwili Hukwama Wakati Akili Imeshaamka?

UKWELI KUHUSU JINAMIZI: KWA NINI MWILI HUKWAMA WAKATI AKILI IMESHAAMKA?

Umewahi kuamka usiku, ukiwa na hakika kabisa kwamba macho yako yamefunguka na akili yako ipo macho kabisa, lakini mwili wako haujibu amri yoyote? Unajaribu kupiga kelele, hakuna sauti inayotoka. Unajaribu kusogeza mkono, mwili unabaki kimya kabisa, kana kwamba kuna kitu kinachokushikilia chini. Wengine huongeza kwamba wanahisi uwepo wa "kitu" kilichowaka karibu, hisia ya woga mkubwa isiyoelezeka. Hali hii, inayojulikana kwa jina la kienyeji kama "jinamizi," ina jina la kisayansi: Sleep Paralysis, au Kupooza kwa Usingizi.

Kisayansi, jinamizi si jambo la kimizimu wala si shambulio la nje, bali ni hali ya kawaida ya kifiziolojia inayotokea pale mipaka kati ya hatua za usingizi na kuamka inapochanganyikana. Ili kuelewa hili vizuri, ni muhimu kwanza kuelewa jinsi usingizi wa binadamu unavyofanya kazi.

Read this on Guava