Ponzi schemes
Katika miaka ya karibuni, Tanzania imeendelea kushuhudia kuibuka kwa mifumo mbalimbali ya uwekezaji inayotoa ahadi za utajiri wa haraka kupitia mtandao. Baadhi ya mifumo hiyo imekuwa ikihusishwa na tabia za Ponzi Scheme, ambapo fedha za wanachama wapya hutumika kulipa wanachama wa zamani badala ya kuzalishwa kupitia biashara halisi. Mfumo huo huendelea kwa muda mfupi kabla ya kuporomoka na kuwaacha maelfu ya watu wakipoteza fedha zao.
Sakata la LBL (Leo Beneath London) limeibua maswali mengi kuhusu uwezo wa taasisi mbalimbali za udhibiti kugundua na kuzuia mifumo yenye viashiria vya udanganyifu kabla haijafikia maelfu ya wananchi. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilieleza wazi kuwa haikuwahi kuipa kampuni hiyo leseni ya kutoa huduma za kifedha, huku BRELA ikifuta usajili wa kampuni kadhaa zilizokuwa zikihusishwa nayo baada ya kubainika kuwa zilikuwa zinaendesha shughuli tofauti na zile zilizosajiliwa awali.
Swali ambalo wengi wanauliza ni hili: Je, mamlaka husika zinapaswa kusubiri mpaka kampuni ianze kufanya makosa ndipo zichukue hatua, au zinapaswa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu Business Model ya kampuni kabla ya kuipa usajili?