Bakteria za Tumboni na Uhusiano Wake na Hisia Zako
Guavah
Tumbo lako si sehemu ya kuchakata chakula tu, ni nyumbani kwa mabilioni ya bakteria wanaoathiri afya yako ya akili. Watafiti sasa huita uhusiano huu "gut-brain axis," yaani njia ya mawasiliano kati ya utumbo na ubongo inayofanya kazi pande zote mbili.
Utumbo na Ubongo Huwasiliana Moja kwa Moja
Utumbo wako umeunganishwa na ubongo kupitia mshipa mkubwa wa fahamu unaoitwa vagus nerve. Hii inamaanisha kuwa hali ya bakteria wako wa tumbo inaweza kuathiri jinsi unavyohisi, na hisia zako pia zinaweza kuathiri jinsi tumbo lako linavyofanya kazi. Ndio maana watu wengi hupata maumivu ya tumbo wanapokuwa na wasiwasi au msongo wa mawazo.